Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

LATRA Logo

Kuendelea Kupatikana kwa Huduma za Teksi Mtandao Nchini
Imewekwa: 17 Aug, 2022

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa mujibu wa Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 ilitangaza viwango vya nauli za teksi mtandao kupitia Gazeti la Serikali Na. 1369 la tarehe 8 Aprili, 2022 na vyombo vingine vya habari.

Pamoja na viwango vya nauli za teksi mtandao, Mamlaka iliweka kiasi cha ukomo wa makato ya asilimia 15 kutoka katika mapato ya dereva kwenda kampuni za teksi mtandao kama kamisheni. Hata hivyo, baadhi ya kampuni za teksi mtandao zilizokuwa zikitoza kamisheni ya asilimia 20 mpaka 31 hazikuridhika na kiwango elekezi cha asilimia 15.

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo