Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kusitisha Ratiba za Mabasi Tisa Yaendayo Mikoani Yanayoanza Safari Saa 9:00 Alfajiri
Imewekwa: 20 Jun, 2023

Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1)(b) na 6(b) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini ina jukumu la kutoa, kuhuisha na kufuta vibali na leseni za usafirishaji na kukuza  usalama kwa sekta zinazodhibitiwa ikiwa ni pamoja na usalama wa watumiaji wa huduma za sekta zinazodhibitiwa. Aidha, katika kuhakikisha Mamlaka yetu inatekeleza majukumu yake ya udhibiti katika usafiri wa abiria, Serikali ilitupatia nyenzo ya udhibiti wa magari na huduma za usafiri wa abiria-Kanuni za Usafirishaji Magari ya Abiria za Mwaka 2020 (Tangazo la Serikali Na. 76 la tarehe 7/2/2020).

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo