Imewekwa: 31 Dec, 2024
Kwa mujibu wa kanuni ya 20(b) ya Kanuni za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Magari ya Kukodi za mwaka 2020, Mabasi Maalumu ya Kukodi (Special Hire) yanapaswa kuunganishwa na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS). Mfumo huo huwezesha Mamlaka kumtambua dereva anayeendesha gari husika endapo dereva huyo atasajiliwa na kutumia Kitufe cha Utambuzi wa Dereva (i-button).