Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Miaka Mitatu ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Ustawi wa Sekta ya Usafiri Ardhini Nchini
Imewekwa: 19 Mar, 2024

Miaka mitatu imetimia tangu Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuingia madarakani. Ilikuwa Ijumaa, Machi 19, 2021 ambapo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliapishwa na Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuanza kuongoza Serikali ya Awamu ya Sita. Siku hii ilikuwa ya kihistoria kwa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais.

Imekuwa ni miaka mitatu yenye matokeo chanya kwa Taifa kwa kuwa Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada za makusudi za kuijenga Tanzania mpya kwa kuweka mbele vipaumbele vya kitaifa kwa maendeleo ya nchi na kusisitiza uzalendo, kuleta umoja, mshikamano, kushirikisha wadau wa maendeleo na kufanya kazi kwa bidii. Kupitia Wizara ya Uchukuzi inayoongozwa na Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Uchukuzi akisaidiwa na Mhe. David Kihenzile, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na Dkt. Ally Possi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi.

Soma zaidi

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo