Imewekwa: 02 Jul, 2025
Kanuni za Tiketi Mtandao za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za mwaka 2024 zilizotangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 20 la Desemba mosi 2024 zimeweka takwa la mifumo ya tiketi mtandao nchini kupata kibali cha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini. Kanuni ya 5 ya Kanuni hizo imeweka vigezo vya kupata kibali ambavyo ni pamoja na mfumo husika kuwa na ulinzi dhidi ya uvamizi wa kimtandao na kuwa na uwezo wa kuunganishwa na mifumo ya Serikali.