Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

LATRA Logo

Mkurugenzi Mkuu atoa Pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Imewekwa: 14 Jul, 2022

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo, ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo kwa magari mawili aina ya Probox na Wish yenye namba za usajili T559 DGU na T 472 DWN, mtawalia, kugongana yakiwa kwenye mwendokasi na kusababisha vifo vya watu watano (5) na majeruhi kumi na mmoja (11).

Katika salamu zake, CPA Suluo ametoa pole kwa wafiwa wote na kuwaombea majeruhi uponaji wa haraka. 

Aidha CPA Suluo amemshukuru mhe. Kafulila kwa ushirikiano anaoipatia Mamlaka hiyo katika udhibiti wa huduma za usafiri mkoani Simiyu na kwa kutoa zuio tarehe 13 Julai 2022 kwa magari madogo maarufu kama ‘mchomoko’ kutoa huduma za kusafirisha abiria kwa masafa marefu kwa kuwa magari hayo si salama kutoa huduma hiyo. 
Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo