Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Mkurugenzi Mkuu LATRA atoa Pole kwa Mkuu wa Mkoa Lindi
Imewekwa: 22 Apr, 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habibu Suluo, ametoa salamu za pole kwa Mhe. Zainab R. Telack, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, kufuatia vifo vya watu 11 na majeruhi 08 vilivyotokana na ajali iliyotokea leo Jumatatu, tarehe 22 Aprili, 2024, majira ya saa 07:30 mchana katika eneo la kijiji cha Somanga, kata ya Somanga, tarafa ya Mitinje, barabara kuu ya Lindi - Kibiti.

Ajali hiyo imehusisha gari la mizigo lenye namba za usajili T224 DZT, aina ya Howo yenye leseni ya LATRA namba C3A316637 iliyotolewa tarehe 15 Julai, 2023 na muda wake utamalizika tarehe 14 Julai, 2024 pamoja na tela lake lenye namba za usajili T920 CUK yenye leseni ya LATRA namba C8A308112 iliyotolewa tarehe 23 Juni, 2023 na muda wake utamalizika tarehe 22 Juni, 2024, mali ya Kampuni ya Speciallised Hauliers Ltd iliyokuwa ikiendeshwa na Bw. Abdallah Hamis Dulazi (37), mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam.

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo