Imewekwa: 09 Dec, 2025
Wizara ya Uchukuzi kwa mujibu wa kifungu cha 45 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, Sura ya 413, inapenda kuwataarifu Wadau wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kuwa, kutakuwa na Mkutano wa Wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu mapendekezo ya kutengeneza Kanuni za Usimamizi wa Madhara ya Uchovu kwa Madereva za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka 2025.

