Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Taarifa ya Mafanikio ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
Imewekwa: 19 Oct, 2023

Ndugu Wahariri na Waandishi wa Habari, kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1)( b) cha Sheria ya LATRA, Mamlaka inao wajibu wa kutoa, kuhuisha, kusitisha na kufuta leseni za usafirishaji, hivyo Mamlaka hutoa leseni kila mwaka kwa vyombo vya usafiri kibiashara. Leseni hizi hutolewa baada ya mtoa huduma kukidhi masharti yanayotakiwa kwa aina ya huduma husika. Leseni hizo hutumika kutambua idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa. Katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2022/23, idadi ya leseni za usafirishaji ziliongezeka kutoka 230,253 hadi 284,158 sawa na ongezeko la leseni 44,205 ambayo ni ongezeko la asilimia 18.4.

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo