Imewekwa: 13 Oct, 2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Amaniel Zakaria Sekulu, Afisa Leseni na Usajili Mwandamizi, Ofisi ya LATRA Mkoa wa Dar es Salaam, kilichotokea asubuhi ya Oktoba 13, 2025 kwa ajali ya barabarani, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, akiwa anaelekea kazini. Bw. Sekulu alikuwa mfanyakazi mahiri, muadilifu na mkweli.