Kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka inajukumu la kusajili wahudumu na kuthibitisha madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara. Aidha, kanuni ya 22(g) ya Kanuni za Magari ya Abiria za Utoaji wa Leseni za Usafirishaji Tangazo la Serikali Na. 76 la Mwaka 2020, imeweka takwa la mtoa huduma kuhakikisha mhudumu anayemwajiri amesajiliwa na LATRA. Vilevile kanuni ya 20(1)(d) ya Kanuni za Uthibitishaji Madereva na Usajili Wahudumu wa Magari ya Biashara za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tangazo la Serikali Na. 81 la Mwaka 2020 zinataka Mhudumu wa Magari ya kibiashara kuwa na Kadi ya Usajili iliyotolewa na Mamlaka.
Imewekwa: 17 May, 2025