Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

LATRA Logo

Utekelezaji wa Mfumo wa Tiketi Mtandao Hadi Tarehe 17.08.2022
Imewekwa: 18 Aug, 2022

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inapenda kuwajulisha wasafiri wanaotumia mabasi ya endayo mikoani na nchi jirani na Umma kwa ujumla kwamba imetekeleza maboresho ya mfumo wa Tiketi Mtandao kwa kushirikiana na wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu Kimtandao (NIDC), Watoa Huduma za Tiketi za Kielektroniki na wadau wengine wa Serikalini na sekta binafsi.

Mamlaka kwa kushirikiana na wadau hao, walifanya kazi ya kuainisha changamoto zilizojitokeza katika mfumo, na baada ya kujiridhisha, wadau wote walikubaliana kutoa muda wa mfumo wa Tiketi Mtandao kufanya kazi kwa majaribio kabla ya kuanza rasmi.

Kipindi cha majaribio kilikua kuanzia tarehe mosi Aprili, 2022 hadi tarehe 30 Juni, 2022. Tarehe mosi Julai, Mamlaka ilitoa muda wa nyongeza wa miezi miwili hadi tarehe 31 Agosti, 2022, ulioambatana na kufanya ukaguzi na kutoa elimu kwa wasafirishaji waliokuwa na changamoto tofauti tofauti ili kuhakikisha mabasi yote yaunganishwe kwenye mfumo huo.

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo