27 Jun, 2023
04:00 asubuhi
Ukumbi wa Mikutano wa Arnaoutoglou
Kwa mujibu wa Kifungu Na 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka ina jukumu la Kusajili Wahudumu na Kuthibitisha Madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara.
Katika kutekeleza jukumu hilo, tarehe 01 Disemba, 2020 LATRA ilianza kusajili madereva husika na tarehe 01 Juni, 2022 walianza kutahiniwa kwa lengo la kuthibitishwa. Aidha, LATRA kwa kushirikiana na vyuo washirika imekamilisha mitaala itakayotumika kutoa mafunzo kwa wahudumu ili Mamlaka ianze kuwasajili.
