Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

MHE. DKT. CHARLES MSONDE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUTOA MAONI YA NAULI ZA MABASI YAENDAYO HARAKA
Imewekwa: 26 May, 2022
MHE. DKT. CHARLES MSONDE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUTOA MAONI YA NAULI ZA MABASI YAENDAYO HARAKA

Na. Mambwana Jumbe

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Dkt. Charles Enock Msonde Mei 26, 2022 amefungua mkutano wa wadau wa kutoa maoni ya nauli za mabasi yaendayo haraka ulioandaliwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Aidha, Mhe. Dkt. Msonde amewataka wadau hao kuwa mabalozi wa dhati katika kuchangia maoni yenye tija kwakuwa maoni yao yatawakilisha wadau wengine ambao hawajapata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo

“Kila mmoja aliyefanikiwa kufika hapa ajuwe kuwa kuna watu wengi anaowawakilisha, hivyo kila mmoja wetu ajitahidi kuwawakilisha ipasavyo”, amesisitiza Mhe. Dkt. Msonde

Naye Mkurugenzi Mkuu LATRA, Bw. Gilliard Ngewe amesema Sheria ya LATRA Na. 3 ya Mwaka 2019, Kifungu Na. 21 Sura ya 413, inaitaka Mamlaka hiyo pindi inapopokea maombi kutoka kwa watoa huduma, kuitisha kikao cha pamoja kwa ajili ya majadiliano kuhusu mapendekezo na hivyo mkutano ulioitishwa wa kukusanya maoni ni wa kisheria.

“Natoa wito kwa wadau mbalimbali kuitumia vizuri nafasi hii, ili kuwawezesha wataalamu wetu wafanye kazi yao kwa ufanisi na ueledi wa hali ya juu”, ameeleza Bw. Ngewe

Bw. Ngewe ameongeza kuwa, kwa wadau ambao wangependa kuwasilisha maoni yao kwa maandishi wanayo nafasi ya kuwasilisha maoni yao kwa maandishi katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu iliyopo katika Jengo la Mamlaka, Barabara ya Nkrumah kabla ya tarehe 07 Juni, 2022, na maoni yanaweza kutumwa kwa barua pepe kupitia anuani hizi: info@latra.go.tz na dg@latra.go.tz

Pakua Hotuba ya Mgeni Rasmi

Pakua Hotuba ya Mkurugenzi Mkuu

 

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo