Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

LATRA YAFANYA KIKAO NA WADAU WA MABASI MAALUM YA KUKODI
Imewekwa: 09 May, 2022
LATRA YAFANYA KIKAO NA WADAU WA MABASI MAALUM YA KUKODI

Na. Mambwana Jumbe

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini tarehe 5 Mei, 2022 imekutana na wadau wa mabasi maalumu ya kukodi na imetoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kuzingatia kabla ya kuanza kutoa leseni za mabasi hayo. 

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara Johansen Kahatano alisema kuwa Mamlaka itaendelea kutoa elimu kwa wadau hao kwa njia mbalimbali ili kujenga uelewa wa pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa watoa huduma na watumia huduma kwa kufuata Sheria na Kanuni.

Kahatano alifafanua kuwa waombaji leseni hizo wanapaswa kuzingatia mambo mbalimbali ya msingi kabla ya kupata leseni ikiwa ni pamoja na basi husika kuunganishwa katika Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi (VTS), kuunganishwa kwenye mfumo wa Tiketi Mtandao na dereva kusajiliwa na LATRA.

Aidha, baada ya kupata leseni msafirishaji anapaswa kuhakikisha kuwa mfumo wa VTS unafanya kazi muda wote, kutoingilia huduma zingine, kutoa tiketi za kielekteoniki na kusoma na kuzingatia Kanuni za Magari ya Kukodi (GN. 78).

Kwa upande wao wadau hao walipata fursa ya kusikiliza mada zilizotolewa na kutoa maoni yaliyopokelewa na LATRA kwa ajili ya kufanyiwa kazi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo