Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

LATRA YAENDESHA WARSHA YA SIKU MBILI KWA WADAU WA USALAMA WA RELI
Imewekwa: 14 May, 2022
LATRA YAENDESHA WARSHA YA SIKU MBILI KWA WADAU WA USALAMA WA RELI

Na. Mambwana Jumbe

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Bw. Gilliard W. Ngewe amewataka wafanyakazi wa Shirika la Reli Nchini (TRC) kutumia maarifa waliyoyapata kwenye warsha ya kupunguza ajali za usafiri wa reli nchini ili kupunguza uwezekano wa ajali katika usafiri huo.


Akizungumza katika warsha hiyo, Bw. Ngewe amesema kuwa, Mamlaka inatekeleza majukumu yake kwa kutoa viwango vya huduma kama vile viwango vya nauli, ukaguzi wa ubora wa miundombinu, na kadhalika ili kumfanya mtoa huduma kutoa huduma bora kwa wananchi.


Naye Meneja wa Raslimali Watu wa TRC, Bw. Humphrey Kong’oke aliishukuru LATRA kwa kuwezesha warsha hiyo na kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupunguza ajali zinazosababishwa na makosa ya kibinadamu.

 Aidha, Bw. Kong’oke amewataka wafanyakazi wa TRC kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa LATRA katika utekelezaji wa kazi zao.

Kwa Upande wake, Afisa Mwandamizi Miundombinu ya Reli – LATRA Mhandisi Lameck Kamando amesema kuwa lengo la Semina hiyo ni kukumbushana juu ya baadhi ya mambo yanayosababisha makosa ya kibinadamu katika usafiri wa reli.

 Pia Mhandisi Kamando amewataka wataalamu wanaopata mafunzo hayo kuwafikishia elimu hiyo wenzao ambao hawakubahatika kushiriki warsha hiyo.
 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo