Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

LATRA MSHINDI WA PILI TUZO ZA NBAA
Imewekwa: 02 Dec, 2024
LATRA MSHINDI WA PILI TUZO ZA NBAA

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeibuka mshindi wa pili katika Tuzo za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kwa uwasilishaji Bora wa Hesabu za Kifedha katika Sekta ya Umma kwa viwango vya Kimataifa (IPSAS) mwaka wa fedha 2022/23 - kundi la Mamlaka za Udhibiti. 

Tuzo hiyo imepokelewa na Bw. Abdallah Mhagama, Kaimu Mkurugenzi Mkuu - LATRA, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa mikutano APC Bunju jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2024.

Ushindi huo ni uthibitisho kuwa LATRA imejipambanua katika misingi ya Uweledi, Uwazi na Uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yake, uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za kifedha.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo