
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeibuka mshindi wa pili miongoni mwa taasisi za Serikali zinazotoa huduma bora na zisizofanya biashara ikiwa ni sehemu ya Serikali kutambua mchango mkubwa wa LATRA katika kuboresha huduma za usafiri ardhini nchini.
Tuzo hiyo imetolewa Agosti 24, 2025 na Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kupokelewa na Prof. Ahmed Ame, Mwenyekati wa Bodi ya LATRA akiambatana na CPA Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu LATRA katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoratibiwa na ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)
Aidha tuzo hiyo imetolewa kwa kuzingatia vigezo vya utawala bora, uboreshaji wa huduma, matumizi ya mifumo ya kidigiti kiwango cha kuridhika kwa wateja pamoja na ongezeko la wananchi wanaonufaika na huduma za LATRA.
LATRA inaendelea kuboresha mifumo, kuongeza ubunifu na kushirikisha wadau ili kuhakikisha wananchi wanafurahia huduma bora, salama na zenye viwango. ushindi huu umechagizwa na jitihada zinazotekelezwa na Bodi ya Wakurugenzi LATRA, Menejimenti pamoja na watumishi wa Mamlaka.