Imewekwa: 09 May, 2022

Na. Mambwana Jumbe
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeridhia kuanza kutumika kwa nauli kikomo za mabasi ya mijini na njia ndefu kutokana na ongezeko la bei ya mafuta ya Petroli na Dizeli lililotokea hivi karibuni.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara Bw. Johansen Kahatano alipokuwa akiongea na wanahabari Mei 06, 2022.
“Tulitangaza nauli kikomo Aprili 30, 2022 ambapo kwa mujibu wa Sheria ya LATRA Na. 3 ya mwaka 2019 na Kanuni zake, nauli hizi zilitakiwa kutumika siku 14 baada ya kuzitangaza. Lakini kutokana na hali halisi ya ongezeko la bei ya mafuta, Mamlaka imeridhia kuanza kutumika kwa nauli hizo”, alifafanua Bw. Kahatano