Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

MKURUGENZI MKUU LATRA ATOA POLE KWA MKUU WA MKOA WA SIMIYU
Imewekwa: 14 Jul, 2022
MKURUGENZI MKUU LATRA ATOA POLE KWA MKUU WA MKOA WA SIMIYU

Na. Mambwana Jumbe

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo, ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo kwa magari mawili aina ya Probox na Wish yenye namba za usajili T559 DGU na T 472 DWN, mtawalia, kugongana yakiwa kwenye mwendokasi na kusababisha vifo vya watu watano (5) na majeruhi kumi na mmoja (11).

Katika salamu zake, CPA Suluo ametoa pole kwa wafiwa wote na kuwaombea majeruhi uponaji wa haraka. 

Aidha CPA Suluo amemshukuru mhe. Kafulila kwa ushirikiano anaoipatia Mamlaka hiyo katika udhibiti wa huduma za usafiri mkoani Simiyu na kwa kutoa zuio tarehe 13 Julai 2022 kwa magari madogo maarufu kama ‘mchomoko’ kutoa huduma za kusafirisha abiria kwa masafa marefu kwa kuwa magari hayo si salama kutoa huduma hiyo. 

“Nawakumbusha wamiliki wote wa vyombo vya usafiri (magari ya abiria -mabasi, daladala, teksi, pikipiki maarufu kama bajaji na bodaboda) na magari ya mizigo vinavyopaswa kuwa na leseni za LATRA wahakikishe wana leseni hai kabla ya kutoa huduma. 

Madereva na Makondakta wanakumbushwa kuvaa sare, kuwa nadhifu wakati wote na kuhakikisha vyombo vyao vinakidhi matakwa ya ubora na usalama”. alisema

Aidha, CPA Suluo aliwataka wamiliki wote wa vyombo vya usafiri wa abiria na mizigo nchini kuhakikisha wana leseni hai za LATRA kuzingatia masharti ya leseni zao wanapotoa huduma. Vile vile amewaomba viongozi katika ngazi zote kushirikiana na LATRA ili kuboresha na kuhakikisha uwepo wa usafiri bora na salama kote nchini.

Mamlaka kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani inaandaa oparesheni maalum ya Ukaguzi na Ufuatiliaji wa vyombo vyote vya usafiri wa abiria na mizigo na itatoa adhabu kali kwa yoyote atakayekiuka masharti ya utoaji wa huduma zinazodhibitiwa.
 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo