Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

TUTUMIE TIKETI MTANDAO KWA MANUFAA YETU SOTE
Imewekwa: 31 Aug, 2022
TUTUMIE TIKETI MTANDAO KWA MANUFAA YETU SOTE

Na Mambwana Jumbe

“Naishukuru Serikali kwa kutuletea tiketi hizi za mtandao kwa sababu nilikuwa napata bugudha sana pindi nilipotaka kusafiri. Ilikuwa nikienda kwenye kituo cha mabasi nagombaniwa kama bidhaa na wakati mwingine kiti kimoja tunakatiwa tiketi zaidi ya mtu mmoja. Basi ilikuwa ni vurugu sana ila kwa mfumo huu mpya wa Tiketi Mtandao kwa kweli mambo yamekuwa rahisi sana. Mimi kwa kutumia simu yangu ya mkononi tu nakata na kulipia tiketi kwa basi ninalolitaka na nachagua kiti ninachokitaka bila shaka yoyote, Halikadhalika, Tiketi Mtandao zinatuondolea uwezekano wa kupandishiwa nauli kiholela” Amina Bakari, mkazi wa Dar es Salaam.

Tiketi Mtandao ni tiketi zinazotolewa kwa njia ya kielekroni ambapo pindi abiria anapokata tiketi hiyo anapata ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu ya mkononi au anapewa risiti kutoka kwenye mashine maalum ikionyesha majina yake na taarifa zake na safari husika. Tiketi hizi ni tofauti na zile tiketi ziizokuwa zikitumika awali ambazo zilikuwa zinaandikwa kwa mkono na kusababisha changamoto kubwa kwa abiria.

Akizungumzia utekelezaji wa mfumo wa tiketi mtandao hadi 17.08.2022, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo amesema hadi sasa jumla ya mabasi 2,033 yanayomilikiwa na kampuni 308 za usafirishaji abiria yameshaunganishwa kwenye mfumo wa Tiketi Mtandao kupitia watoa huduma (vendors). “Hadi kufikia Agosti 17, 2022, Jumla ya mabasi 7,649 yamesajiliwa kwenye Mfumo wa Ufuatiliaji Mwenendo wa MagariVTS ambapo mabasi 3,916 yameonekana yapo barabarani (active). Mafanikio haya ni sawa na asilimia 52 ukilinganisha na asilimia 37 ilivyokuwa Julai 31, 2022.”

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo