Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

UTHIBITISHAJI WA MADEREVA NI TIJA YA KUBORESHA USALAMA NA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI NCHINI
Imewekwa: 15 Sep, 2022
UTHIBITISHAJI WA MADEREVA NI TIJA YA KUBORESHA USALAMA NA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI NCHINI

Na. Mambwana Jumbe

Ulishawahi kujiuliza ni madhara gani yanatokana na ajali za barabarani au taabu wanazopitia waathirika wa ajali? Na je, vipi kuhusu familia zinazobaki baada ya kupoteza wapendwa wao kama athari za ajali hizo?

Watu wengi hupitia wakati mgumu na kushindwa kuendelea na shughuli zao za kila siku kutokana na athari za moja kwa moja zinazotokana na ajali za barabarani mathalani kuwa majeruhi, kupata ulemavu wa maisha au hata kupoteza maisha. Athari hazipo tu kwa abiria wanaotumia vyombo hivyo vya usafiri pindi wanapopata ajali, bali kwa wamiliki wa vyombo pia hupata hasara kwa kuharibikiwa vyombo vya usafiri, Serikali hupata hasara kwa uharibifu wa miundombinu ya barabara na kuingia gharama za kufanya matengenezo.Mzigo huu hubebwa nasi sote kama Taifa tunapolazimika kutumia fedha za kigeni kununua magari mapya kama mbadala wa magari yaliyopata ajali, kununua vipuri na madawa kwa ajili ya kutibia majeruhi wa ajali hizo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu TAKWIMU YA HALI YA UHALIFU NA MATUKIO YA USALAMA BARABARANI ya mwaka 2020, asilimia 91 ya ajali zinazotokea Tanzania Bara zinatokana na uzembe na makosa ya kibinadamu kama vile uendeshaji wa hatari, uzembe wa watumiaji wa barabara, mwendokasi na ulevi. Takwimu hizo zinaonesha vyanzo vingine vya ajali kuwa ni asilimia 5.7 inayochangiwa na ubovu wa vyombo vya moto na asilimia 2.7 inayochangiwa na sababu za kimazingira kama vile moto, vizuizi vya njia pamoja na ubovu wa barabara.

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo