Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Hotuba ya Mkurugenzi Mkuu (LATRA) katika Hafla ya Utoaji wa Vyeti kwa Madereva wa Vyombo vya Moto Vinavyotoa Huduma Ya Usafiri Kibiashara Waliofanya Mtihani na Kuthibitishwa.
Imewekwa: 01 Jul, 2023

Awali ya yote natoa shukrani za kipekee kwa Mheshimiwa Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, kwako Mheshimiwa Atupele F. Mwakibete (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Gabriel J. Migire, Katibu Mkuu (Uchukuzi) na Dkt. Ally Possy, Naibu Katibu Mkuu (Uchukuzi) kwa kazi kubwa mnayoifanya ya ujenzi wa taifa na kiupekee kabisa, jinsi mnavyoiwezesha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni.

 

Mheshimiwa Mgeni Rasmi

Kiupekee kabisa nakushukuru wewe kwa kukubali ombi letu na kujumuika nasi siku hii ya leo katika shughuli hii muhimu ya utoaji wa vyeti kwa madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma ya usafiri kibiashara waliofanya mtihani na kuthibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) pamoja na kuzindua rasmi mitaala itakayotumika kutoa mafunzo kwa wahudumu magari ya kibiashara. Tunafahamu kuwa unayo majukumu mengi na makubwa yenye maslahi makubwa kwa Taifa, hata hivyo umeweza kutenga muda wako na kufika hapa ili kutimiza jukumu hili ambalo pia ni la maslahi makubwa kwa Watanzania na Taifa letu kwa jumla.

 

Mheshimiwa Mgeni Rasmi

Pia, natoa shukrani za dhati kwa wadau wote waliopo hapa kwa kukubali mialiko yetu na kuhudhuria hafla hii. Ninatambua kila mmoja wetu ana majukumu mazito ya kiofisi au binafsi lakini kwa kutambua umuhimu wa mjumuiko huu ameacha shughuli zake ili kwa pamoja tuweze kushirikiana.

Pakua hotuba

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo