Imewekwa: 23 Jun, 2025
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inaendelea kusimamia utekelezaji wa Kanuni za Tiketi Mtandao za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za mwaka 2024 zilizotangazwa katika Gazeti la Serikali Na. 20 la tarehe 12 Januari 2024. Kwa mujibu wa Kanuni hizo, watoa huduma za mifumo ya tiketi mtandao wanapaswa kuwa wameidhinishwa na LATRA.