Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kuomba Cheti cha Uwakala wa LATRA
Imewekwa: 15 Jun, 2026

Muombaji atatuma maombi katika mfumo wa RRIMS na ndani ya saa 24 atakuwa amepatiwa namba ya malipo ya cheti chake cha uwakala.  

 

Hatua za kufuata

i.  Ingia katika mfumo wa RRIMS kwa kufungua kiunganishi ‘link” rrims.latra.go.tz   

ii.  Sajili akaunti (ikiwa hauna akaunti katika mfumo wa LATRA)

iii.  Ingia kwenye akaunti yako kwa barua pepe uliyoitumia kujisajili.

iv.  Nenda kwenye sehemu ya Maombi ya Cheti.

v.  Anza maombi kwa kubonyeza kitufe cha “Ongeza Maombi.

vi.  Jaza taarifa zote zinazohitajika, ikiwemo aina ya Cheti, ambapo utachagua uwakala (Authorised Agent)

vii.  Ambatisha nyaraka na kutuma maombi

viii.  Mara baada ya kutuma, fuatilia maombi yako kupitia mfumo

ix.  Baada ya hatua hii, namba ya malipo itatumwa kwa wakala kupitia namba yake ya simu.

 

Ada na Malipo ya Cheti

i.  Ada ya leseni ya Uwakala Sh. 200,000/= kwa mwaka;

ii.  Ada ya leseni ya Uwakala kwa Kampuni za Kigeni USD 200 kwa mwaka;

iii.  Fomu ya maombi Sh. 50,000/= kwa Mawakala wa ndani na USD 50 kwa Mawakala wa Kigeni

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor