Vigezo/Sifa za Mwombaji
i. Mtu binafsi
ii. Kampuni
iii. Taasisi ya Serikali
iv. Chama cha ushirika
Taratibu za Kufuata
Mtu Binafsi
a. Awe na nakala ya kitambulisho cha Uraia
b. Awe na namba ya mlipakodi (TIN)
c. Nyaraka nyingine ambazo Mamlaka itazihitaji
Kampuni
a. Awe na nakala ya leseni ya biashara
b. Awe na namba ya mlipakodi (TIN)
c. Awe na cheti cha usajili kwa kampuni.
d. Awe na nakala ya umiliki wa ofisi au makubaliano ya pango.
e. Awe na mpango wa biashara ya Uwakala;
f. Awe na cheti cha Uthibitisho wa kulipa Kodi;
g. Awe na nyaraka nyingine ambazo Mamlaka itazihitaji.
Kwa Taasisi ya Serikali
a. Iwe na namba ya mlipakodi (TIN)
b. Iwe na nyaraka nyingine ambazo Mamlaka itazihitaji.
Kwa Chama cha Ushirika
a. Kiwe na nakala ya umiliki wa ofisi au makubaliano ya pango;
b. Kiwe na cheti cha usajili wa SACCOS
c. Kiwe na cheti cha uthibitisho wa kulipa kodi
d. Kiwe na nyaraka nyingine ambazo Mamlaka itazihitaji

