Nyaraka zinazohitajika
Kadi ya usajili wa Pikipiki
Hatua za Kufuata
a) Kupata linki ya mfumo, ingia kwenye tovuti ya Mamlaka www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )
b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe na nywila yako kwenye sehemu husika,
c) Chagua neno lililoandikwa Maombi ya leseni, bofya sehemu iliyoandikwa Bodaboda/ Bajaji
d) Chagua neno Ongeza gari
e) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika, ambatisha nakala ya Kadi ya pikipiki kisha wasilisha maombi hayo kwenye ofisi ya LATRA uliyochagua
f) Maombi ya leseni yatashughulikiwa ndani ya saa ishirini na nne (24)
g) Msafirishaji utapata ankara ya Malipo (Control number)
h) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number) kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa,Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k) benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)
i) Baada ya malipo unaweza kuchapa leseni yako mtandaoni kupitia akaunti yako ya RRIMS.
Zingatia
Hatua za maombi ya leseni, zitafuatwa na waombaji wa leseni wanaohuisha leseni, kubadili njia/huduma/ratiba baada ya mwombaji wa leseni kuchagua huduma anayohitaji.
Uhai wa Leseni: Mwaka mmoja
Gharama za maombi ya leseni
Unapotuma maombi ya leseni gharama yake TZS. 2,000/= au Dola 5
Gharama za leseni
- Leseni ya Pikipiki magurudumu mawili TZS. 15,000/= au Dola 20
- Leseni ya Pikipiki magurudumu matatu TZS. 20,000/= au Dola 20
Zingatia
Malipo yote yafanyike kwa ankara ya malipo (control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo iliyotolewa na Mamlaka.