Nyaraka zinazohitajika
a) Kadi ya usajili wa gari;
b) Hati ya Bima iliyo hai;
c) Hati ya ukaguzi wa gari kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na risiti yake ya malipo.
Hatua za Kufuata
a) Kupata linki ya mfumo, ingia kwenye tovuti ya Mamlaka www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )
b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe na nywila yako kwenye sehemu husika,
c) Chagua neno lililoandikwa Maombi ya leseni, bofya Maombi ya Leseni Magari ya Mizigo,
d) Chagua neno Ongeza gari,
e) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika, ambatisha nakala za vielelezo vinavyohitajika kisha, wasilisha maombi hayo kwenye ofisi ya LATRA uliyochagua,
f) Maombi ya leseni yatashughulikiwa na Maafisa leseni ndani ya saa ishirini na nne (24),
g) Msafirishaji utapata ankara ya malipo (Control number)
h) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number) kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa, Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k) benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)
i) Baada ya malipo unaweza kuchapa leseni yako mtandaoni kupitia akaunti yako RRIMS.
Zingatia
Hatua za maombi ya leseni, zitafuatwa na waombaji wa leseni wanaohuisha leseni baada ya mwombaji wa leseni kuchagua huduma anayohitaji.
Uhai wa Leseni: Mwaka mmoja
Gharama
- Unapotuma maombi ya leseni gharama yake ni TZS. 20,000/=
- Gharama ya kubadili taarifa za mmiliki ni TZS. 30,000/=
- Gharama ya kuvuka mpaka ni TZS. 200,000/=
- Gari lenye uzito usiozidi tani moja TZS. 50,000/=
- Gari lenye uzito tani 1 na usiozidi tani 5 TZS. 80,000/=
- Gari linalozidi tani 5 na lisilozidi tani 10 TZS. 120,000/=
- Gari linalozidi tani 10 na lisilozidi tani 15 TZS. 150,000/=
- Gari linalozidi tani 15 na lisilozidi tani 20 TZS. 200,000/=
- Gari linalozidi tani 20 na lisilozidi tani 25 TZS. 250,000/=
- Gari linalozidi tani 25 na lisilozidi tani 30 TZS. 280,000/=
- Gari linalozidi tani 30 na kuendelea TZS. 300,000/=
- Trela au Semi Trela linalozidi tani 30 na kuendelea TZS. 300,000/=
- Kichwa cha Lori (Horse/ Tractor) linalozidi tani tani 5 na lisilozidi tani 10 TZS. 120,000/=
Zingatia
Malipo yote yafanyike kwa ankara ya malipo (Control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo iliyotolewa na Mamlaka

