Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

MHE. MTAKA AIPONGEZA LATRA
Imewekwa: 06 Aug, 2023
MHE. MTAKA AIPONGEZA LATRA

Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa Njombe ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kusaidia kuondosha malalamiko yasiyo ya msingi kwa wasafirishaji nchini na kuleta suluhu badala ya malumbano.

Mhe. Mtaka ameyasema hayo Agosti 5, 2023 alipotembelea banda la LATRA katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Aidha, Mhe. Mtaka ameipongeza LATRA kwa kujitangaza ndani ya muda mfupi tangu kuanzishwa kwake ambapo imekuwa miongoni mwa taasisi zenye hadhi kubwa nchini kutokana na namna inavyotekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi.

Vilevile Mhe. Mtaka ameisihi LATRA kuwekeza kwenye ubunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwatumia vijana ili kutengeneza mifumo itakayorahisisha zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma za usafiri ardhini kwa kuwa teknolojia inaleta suluhisho katika masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtaka ameitaka LATRA kuwa washauri wazuri kwenye miundombinu mipya inayojengwa na Serikali kwenye maeneo ya usafiri. Pia ameshauri kwenye maeneo ya stendi pale abiria wanaposubiri waone masuala ya msingi yanayohusu usafiri kwa njia ya mtandao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu LATRA CPA Habibu Suluo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano LATRA Bw. Salum Pazzy, alimshukuru Mhe. Mtaka kwa miongozo aliyoitoa na kuwa Mamlaka imeshafunga runinga maalumu katika Kituo cha Mabasi Magufuli na Kituo cha Nanenane Dodoma kwa ajili ya kuonesha taarifa mbalimbali za abiria.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo