Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

KATIBU MKUU - UCHUKUZI AMKABIDHI OFISI MKURUGENZI MKUU MPYA LATRA
Imewekwa: 11 Jul, 2022
KATIBU MKUU - UCHUKUZI AMKABIDHI OFISI MKURUGENZI MKUU MPYA LATRA

Na. Mambwana Jumbe

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire amemkabidhi ofisi Mkurugenzi Mkuu mpya wa LATRA Bw. Habibu J. Suluo leo tarehe 11 Julai, 2022 baada ya kufanya kikao na menejimenti ya LATRA katika ukumbi wa Makao Makuu ya LATRA jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Bw. Migire amewasihi wafanyakazi wa LATRA kuchapa Kazi kwa juhudi na maarifa ili kufikia matarajio ya Wizara na Serikali kwa ujumla katika kutoa huduma kwa wananchi hususan katika kuboresha ufanisi wa mfumo wa Tiketi Mtandao na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi (VTS).

“LATRA ina nafasi kubwa katika Sekta ya Usafiri Ardhini, na ikifanya kazi vizuri itachangia sana ukuaji wa uchumi, hivyo Serikali na Wizara inamatarajio makubwa kwa Mamlaka hii.” ameeleza.

Aidha Katibu Mkuu amesisitiza LATRA kufanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali ili kushirikiana kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya usafiri ardhini.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu LATRA Habibu Suluo amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua na kuwa amepokea uteuzi huo kwa heshima na kumshukuru Mkurugenzi Mkuu aliyemaliza muda wake Bw. Gilliard Ngewe kwa mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka wakati wa uongozi wake.

Aidha, Bw. Suluo ameahidi kufanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa LATRA ambao kwa kiasi kikubwa anawafahamu kwa muda mrefu aliowahi kufanyanao kazi.

Aliongeza kuwa, anazifanahamu changamoto nyingi za usafiri ardhini, hivyo atashirikiana na timu ya wafanyakazi wa LATRA kuzitatua changamoto hizo, kuendeleza mazuri yaliyoanzishwa na kuboresha zaidi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire amemkabidhi ofisi Mkurugenzi Mkuu mpya wa LATRA Bw. Habibu J. Suluo leo tarehe 11 Julai, 2022 baada ya kufanya kikao na menejimenti ya LATRA katika ukumbi wa Makao Makuu ya LATRA jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Bw. Migire amewasihi wafanyakazi wa LATRA kuchapa Kazi kwa juhudi na maarifa ili kufikia matarajio ya Wizara na Serikali kwa ujumla katika kutoa huduma kwa wananchi hususan katika kuboresha ufanisi wa mfumo wa Tiketi Mtandao na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi (VTS).

“LATRA ina nafasi kubwa katika Sekta ya Usafiri Ardhini, na ikifanya kazi vizuri itachangia sana ukuaji wa uchumi, hivyo Serikali na Wizara inamatarajio makubwa kwa Mamlaka hii.” ameeleza.

Aidha Katibu Mkuu amesisitiza LATRA kufanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali ili kushirikiana kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya usafiri ardhini.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu LATRA Habibu Suluo amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua na kuwa amepokea uteuzi huo kwa heshima na kumshukuru Mkurugenzi Mkuu aliyemaliza muda wake Bw. Gilliard Ngewe kwa mafanikio yaliyofikiwa na Mamlaka wakati wa uongozi wake.

Aidha, Bw. Suluo ameahidi kufanya kazi kwa ukaribu na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa LATRA ambao kwa kiasi kikubwa anawafahamu kwa muda mrefu aliowahi kufanyanao kazi.

Aliongeza kuwa, anazifahamu changamoto nyingi za usafiri ardhini, hivyo atashirikiana na timu ya wafanyakazi wa LATRA kuzitatua changamoto hizo, kuendeleza mazuri yaliyoanzishwa na kuboresha zaidi.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo