Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

LATRA YAPONGEZWA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026
Imewekwa: 18 Jun, 2026
LATRA YAPONGEZWA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026

Bw. Biseko Chiganga, Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Uchukuzi, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa juhudi za kudhibiti huduma za usafiri ardhini pamoja na kusimamia utekelezaji wa sheria za usafirishaji nchini.

Bw. Chiganga ametoa pongezi hizo Juni 16, 2026, alipotembelea banda la LATRA katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, jijini Dodoma, ambapo alipatiwa elimu  kuhusu majukumu ya LATRA pamoja na mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayotumiwa na Mamlaka.

Pia amesema kazi za kiudhibiti zinazofanywa na LATRA zimechangia kuimarisha utoaji wa huduma zenye ufanisi na zinazozingatia sheria huku akisisitiza matumizi ya mifumo ya TEHAMA na kanuni za usafirishaji haswa katika sekta ya Reli.

“Kupitia mifumo ya TEHAMA imewarahisishia utekelezaji wa majukumu ya udhibiti wa  usafiri na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi na niwapongeze kwa juhudi zenu kubwa mnazozifanya katika sekta ya Reli kuanzia kupanga nauli ya daraja la kawaida mpaka utoaji wa huduma mmezingatia hali halisi ya wananchi wa Tanzania” amesema Bw. Chiganga

Kwa upande wake Bw. Salum Pazzy Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano LATRA amesema mifumo ya TEHAMA imerahisisha ufanisi na utendaji kazi wa Mamlaka ikiwemo Mfumo wa Taarifa kwa Abiria (PIS) unaomuwezesha mwananchi kutambua muda basi la masafa marefu kufika pamoja na kufahamu mwendo kasi wa basi likiwa safarini.

“LATRA imejipambanua kwenye mifumo mbalimbali ya TEHAMA ikiwemo Mfumo wa PIS ambao ni Mfumo unaomwezesha mwananchi kupata taarifa za muda wa basi la masafa marefu kufika katika stendi husika, mwendo kasi wa basi pamoja na eneo basi lilipo kwa wakati huo” amesema Bw. Pazzy

LATRA itaendelea kutoa elimu kwa wadau mbali mbali kuhusu kazi na majukumu ya Mamlaka katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23, 2026 Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma, yakibeba kaulimbiu isemayo, “Kuchochea Uwajibikaji Jumishi kwa Huduma Endelevu.”

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo

slot gacor