Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

MABASI 550 YAUNGANISHWA KWENYE MFUMO WA TIKETI MTANDAO
Imewekwa: 27 Jul, 2022
MABASI 550 YAUNGANISHWA KWENYE MFUMO WA TIKETI MTANDAO

Na. Mambwana Jumbe

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo amesema mfumo wa tiketi mtandao kwa mabasi ya masafa marefu umeanza kutumika rasmi Julai, 2022 ambapo hadi sasa jumla ya mabasi 550 yameshaunganishwa kwenye mfumo huo na kwa siku yanakatisha wasitani wa tiketi 5,000 – 7,000.

CPA Suluo amesema hayo kwenye kikao na waandishi wa habari kilichofanyika Dodoma Julai 26, 2022.

“Baada ya kikao cha tathmini tulichofanya hivi karibuni, sisi LATRA, TRA na TABOA tumeazimia kwa pamoja kuwa kufikia mwisho wa mwezi huu wa Julai mabasi yote yawe yameunganishwa kwenye mfumo na yanatoa tiketi za kieletroniki”, amesema CPA Suluo.

Aidha, ameongeza kuwa, matumizi ya tiketi za kieletroniki yamelenga kuwanufaisha wasafirishaji, abiria na Serikali, na Kupitia mfumo huo wasafirishaji wanaweza kudhibiti mauzo ya tiketi kwa kuwa mfumo unawawezesha kuona mauzo yote yanayofanyika kupitia simu za mkononi.

“Ni matarajio yetu kuwa matumizi ya mfumo yatawawezesha wasafirishaji kuimarisha huduma zao kwa kuongeza uwekezaji kwenye sekta. Abiria watanufaika na matumizi ya mfumo kwa kuwezeshwa kukata tiketi kutokea mahali popote na kuepukana na adha za wapiga debe”, amefafanua

Vilevile amesema, Serikali itanufaika kwa taarifa zinazozalishwa na mfumo kwa kupata taarifa mbali mbali zitakazosaidia kufanya maamuzi muhimu yakiwemo ya kuboresha huduma, miundombinu na kukokotoa kodi ya mapato.

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo