Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

MHE. PROF. MBARAWA : ASHUHUDIA SHUGHULI ZA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI ZINAZOTEKELEZWA NA LATRA
Imewekwa: 18 Oct, 2024
MHE. PROF. MBARAWA : ASHUHUDIA SHUGHULI ZA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI ZINAZOTEKELEZWA NA LATRA

Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), Waziri wa Uchukuzi,  ametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Kimataifa wa Lojistiki na Uchukuzi, na kushuhudia shughuli za Udhibiti Usafiri Ardhini zinazotekelezwa na LATRA.

Akitoa maelezo katika banda la LATRA, Bw. Abdallah Mhagama, Kaimu Mkurugenzi Mkuu LATRA,  amesema kuwa, LATRA imeongeza ufanisi katika huduma zinazodhibitiwa kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ikiwa ni pamoja na Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) ,Mfumo wa Taarifa kwa Abiria (PIS) unaomuwezesha abiria kujua basi lilipo, muda wa kuwasili kituoni na kukagua mwendo kasi wa basi, pamoja na maboresho yaliyofanyika kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za  Barabara na Reli  (RRIMS) ambao unamuwezesha mtoa huduma kupata leseni kiganjani mwake bila ulazima wa kufika ofisini.

Vilevile Bw. Mhagama  ameishukuru Wizara ya Uchukuzi kwa kupitisha kanuni nane (8) za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri  Ardhini ( LATRA ) zinazoenda kuleta manufaa kwa Nchi na Taasisi kwa ujumla.

Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Dar es Salaam, kwanzia Oktoba 17 hadi 19, 2024.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo