Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

UWADAJA MBIONI KUANZISHA USHIRIKA
Imewekwa: 08 Jun, 2025
UWADAJA MBIONI KUANZISHA USHIRIKA

DCP Johansen Kahatano, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), amekutana na viongozi na wajumbe wa Umoja wa Daladala Jiji la Arusha (UWADAJA) kwa lengo la kufahamu hatua waliofikia ya kuanzisha chama cha ushirika cha wamiliki wa daladala Mkoani humo, Juni 06, 2025.

Vilevile, DCP Kahatano amewapongeza UWADAJA kwa hatua nzuri waliofikia katika uanzishaji wa ushirika wa chama chao na kuwaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha umoja huo unaoanzisha chama cha ushirika ambacho kitakuwa na msaada kwao wa kiuchumi na kuwawezesha kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wanachama na ushirika kwa jumla.

“Ushirika mtakaoanzisha utawawezesha kutoa huduma za usafiri kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia ueledi kutokana na nguvu ya kiuchumi katika kumiliki vyombo vikubwa na vya kisasa, kuajiri wataalamu wa fani husika na kuzingatia Sheria katika utoaji huduma,” ameeleza DCP Kahatano.

Kwa upande wake Bw. Alibano Matemwa, Mwenyekit wa UWADAJA amesema umoja wao ulilenga kujiinua kiuchumi na kijamii, “Ili kutekeleza malengo haya, ilitupasa kufikiria kuwa na taasisi yenye uwezo wa Kisheria hivyo kwa pamoja tukaamua kuanzisha ushirika, maana ni rahisi wa kuundesha pia unatoa nafasi sawa kwa kila mjumbe kushirki katika kutoa mawazo, maboresho na tunaamini sote tutanufaika na ushirika wetu kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo kwa ajili yetu na familia zetu,” amesema Bw. Matemwa

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi ya UWADAJA jijini Arusha na kuhudhuriwa na Bw. Omary Saleh Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Arusha pamoja na Wajumbe wa UWADAJA.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo