Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Nauli za mabasi ya mjini

Amri ya Bodi ya LATRA iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali (Taarifa ya Kawaida Na. 6935), Toleo Na. 47 la tarehe 24 Novemba, 2023 ni kama ifuatavyo:

Kifungu cha 19 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini, Sura ya 413 imeipa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) jukumu la kupanga na kufanya marejeo ya tozo za huduma ya usafiri ikiwa ni pamoja na nauli za mabasi.

Mamlaka inautangazia umma kuhusu marejeo ya nauli za mabasi ya mijini kama zinavyoonekana kwenye Jedwali hapa chini,

NAULI ZA MABASI YA MIJINI (DALADALA)

Na.

Umbali wa Njia

Nauli (SH.)

1

Usiozidi Kilomita 10

600

2

Kuanzia Kilomita 11 hadi 15

700

3

Kuanzia Kilomita 16 hadi 20

800

4

Kuanzia Kilomita 21 hadi 25

900

5

Kuanzia Kilomita 26 hadi 30

1,100

6

Kuanzia Kilomita 31 hadi 35

1,300

7

Kuanzia Kilomita 36 hadi 40

1,400

 

Nauli ya Mwanafunzi

Nauli ya mwanafunzi kwa mabasi ya mijini (daladala) kwa umbali wa njia zote itaendelea kuwa shilingi 200 kwa kila safari.

MAMBO YATAKAYOFUATILIWA NA LATRA

LATRA inawaelekeza watoa huduma wa usafiri wa mabasi ya masafa marefu na mijini (daladala) kuzingatia yafuatayo:

  1. Nauli zinazotozwa zisizidi ambazo zimetolewa kwenye Tangazo hili.
  2. Madereva na wahudumu (makondakta) kuvaa sare safi na nadhifu.
  3. Mtoa huduma kutotoza nauli zaidi ya umbali anaoenda abiria.
  4. Basi liwe safi wakati wote na kupuliza dawa ya kuua wadudu.
  5. Nauli ziandikwe ubavuni mwa gari upande wa mlango wa kuingia abiria.
  6. Kutokatisha njia (route) ya safari.
  7. Kutokuweka miziki na/au nyimbo na picha (video) zilizo kinyume na maadili ya Kitanzania.
  8. Kuzuia mahubiri ya aina yoyote na kuzuia kufanya biashara ndani ya basi.
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo