Wiki ya Huduma kwa Wateja ni tukio linaloangazia umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na nafasi ya watoa huduma katika kujenga uhusiano mzuri na wateja. Maadhimisho haya yanatoa fursa kwa taasisi na mashirika mbalimbali kutafakari namna ya kuboresha huduma, kuongeza ubunifu na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi na kuzidi matarajio ya wateja.
Kwa kutambua mchango na umuhimu wa wateja katika kuboresha Sekta ya Usafiri Ardhini, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inaungana na wadau wengine kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026, kwa kuzingatia kaulimbiu “Extra Mile”, yaani “Kufanya Zaidi ya Kinachotarajiwa.”

