Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Hotuba ya Mkurugenzi Mkuu (LATRA) Katika Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Treni ya Abiria Dar Es Salaam
Imewekwa: 19 Aug, 2022

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima, afya na fursa ya kuweza kukutana hapa leo ili kupokea mapendekezo ya mabadiliko ya nauli za usafiri wa treni, kuyajadili, kutoa mapendekezo na kasha kumpa fursa Mdhibiti (LATRA) kufanya tathmini ya mapendekezo hayo kwa kuzingatia taarifa iliyo wasilishwa na maoni ya wadau.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Pili, natoa shukrani za kipekee kwako kwa kukubali ombi letu na kujumuika nasi katika shughuli hii muhimu ya kupokea maoni ya wadau wa usafiri wa treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda vituo vya nje ya Dar es Salaam.

Tunafahamu kwamba unayo majukumu mengi, makubwa na muhimu katika ratiba zako, lakini pia umeweza kutenga muda na kufika hapa ili kutimiza jukumu hili ambalo pia ni la maslahi makubwa kwa Watanzania na Taifa letu kwa ujumla.

Hii ni bishara njema kwetu, wadau tuliopo hapa na Watanzania wote. Mheshimiwa Mgeni Rasmi, naomba pia naomba nitoe shukrani zangu za dhati na za moyoni kwa wadau wetu wote na hasa waliopo hapa kwa kukubali mwaliko wetu na kuhudhuria mkutano huu.

Ninatambua kila mmoja wetu ana majukumu mazito ya kiofisi au hata ya binafsi lakini kwa kutambua umuhimu wa mkutano huu wameacha shughuli zao ili kwa pamoja tuweze kushirikiana katika hili.

Pakua hotuba 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo