Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

LATRA Inaendelea Kutekeleza Majukumu ya Udhibiti kwa Mujibu wa Sheria
Imewekwa: 16 Jun, 2025

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inautaarifu Umma kwamba, tarehe 05 Juni, 2025, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali, ikiwemo Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413 na Sheria ya Utoaji wa Leseni Sura ya 317.

Marekebisho hayo yameondoa majukumu ya Ukaguzi wa Utimamu wa Magari (roadworthness) na Uratibu wa shughuli za Usalama wa Usafiri Ardhini katika Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini. Ukaguzi wa Magari ulioondolewa ulikuwa unalenga kuwa na mfumo wa kisasa wa ukaguzi wa lazima wa magari yanayotoa huduma kibiashara kabla ya magari hayo kupewa leseni za LATRA.

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo