Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Taarifa Kwa Umma Kwa Watoa Huduma Watakaokiuka Masharti Ya Leseni za Usafirishaji Abiria Mijini (DALADALA)
Imewekwa: 17 Oct, 2023

Mamlaka imebaini uwepo wa baadhi ya watoa huduma za usafiri wa abiria mijini (daladala) waliokusudia kupandisha nauli za usafiri huo kiholela kwa madai ya kupanda kwa bei ya mafuta (diseli na petrol). Pamoja na LATRA kukutana na watoa huduma hao kwa kuwaelimisha juu ya utaratibu unaopasa kufuatwa kisheria, baadhi yao wameonesha nia ya wazi kupinga na wamekusudia kukiuka masharti ya leseni zao kwa kupandisha nauli kiholela. Azma hii ovu haikubaliki katika Nchi yetu hasa kipindi hiki ambacho, Serikali yetu sikivu kupitia LATRA, imeanza kushughulikia maombi ya kufanya marejeo ya nauli. Kwa mujibu wa kanuni ya 30 ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji (Mabasi ya Abiria) za Mwaka 2020 (Tangazo la Serikali Na. 76 la tarehe 7/2/2020), ni kosa kutoza nauli zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Amri ya LATRA iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 8 la tarehe 6 Mei, 2022, iliweka viwango vya nauli kwa mabasi ya mijini (daladala), ambavyo bado havijabadilika, kama ifuatavyo:

 

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo