28 May, 2024
3:00 asubuhi
Ukumbi wa Mikutano wa Arnaoutouglou
Kwa mujibu wa Kifungu Na. 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka ina jukumu la Kusajili Wahudumu na Kuthibitisha Madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara.
Katika kutekeleza jukumu hilo, tarehe 01 Disemba, 2020 LATRA ilianza kusajili madereva husika na tarehe 01 Juni, 2022 walianza kutahiniwa kwa lengo la kuthibitishwa. Aidha, Julai 01, 2023 jumla ya madereva 999 walitunukiwa vyeti vya uthibitisho vya LATRA baada ya kufanya mtihani na kufaulu.