06 Apr, 2026
3:30 asubuhi
Karimjee Hall, Dar es Salaam
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa kuzingatia Kifungu cha 19 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413 huandaa na kufanya mapitio ya tozo mbalimbali za huduma za usafiri ardhini zinazodhibitiwa ikiwemo nauli za usafiri wa umma kwa njia ya Barabara. Uandaaji wa tozo hizo huzingatia mazingira mbalimbali ikiwemo maslahi ya Watumia Huduma na Watoa Huduma. Katika kipindi cha hivi karibuni, kumetokea ongezeko la bei ya mafuta (petroli na dizeli) kwa takribani Shilingi za Kitanzania 950 kwa lita moja.

