Endapo hujaridhika na huduma uliyoipata kwa mtoa huduma za usafiri ardhini ni haki yako kuwasilisha malalamiko kwa kufuata utaratibu ufuatao:
Kwa Mtoa Huduma
a. Wasilisha malalamiko yako kwa mtoa huduma husika ndani ya siku 7 tangu tarehe ya kutoridhika.
b. Mtoa huduma atashughulikia malalamiko yako na kutoa uamuzi ndani ya siku 21
c. Endapo malalamiko yatakataliwa, sababu zitatolewa kwa maandishi.
Endapo hujaridhika na jinsi malalamiko yako yalivyoshughulikiwa, wasilisha malalamiko hayo kwa Mamlaka kwa utaratibu ufuatao;
Kwa Mamlaka
a. Wasilisha malalamiko kwa Mamlaka ndani ya siku 14 tangu siku uliyopokea majibu kutoka kwa mtoa huduma.
b. Utapewa au utapakua Fomu ya Kuwasilisha Malalamiko ya kujaza.
c. Ambatisha nyaraka zinazohitajika kwenye fomu ya malalamiko
d. Wasilisha fomu kwa baruapepe info@latra.go.tz au kwa kufika ofisi za LATRA zilizo karibu yako.
Utaratibu wa Mamlaka wa Kushughulikia Malamiko
a. Mamlaka itapitia na kutathmini Malalamiko yatapitiwa na kutathminiwa.
b. Usuluhishi utafanyika ndani ya siku 14 endapo malalamiko yana msingi.
c. Yasipotatuliwa, yatawasilishwa kwa ngazi ya juu kwenye kwenye Kamati ya Kushughulikia Malalamiko kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu.

