Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Hotuba ya Mkurugenzi Mkuu LATRA CPA Habibu Suluo kwa Wafanyakazi wa TRC Septemba 26, 2022 DODOMA
27 Sep, 2022 Pakua

LATRA, katika majukumu yake muhimu katika udhibiti usafiri wa reli, ni pamoja na kusimamia usalama pia ufanisi katika uendeshaji wa reli (TRC) na hivyo ikibaini mapungufu, kuchukua hatua stahiki haraka iwezekanavyo. Katika kudhibiti usafiri wa reli TRC, taarifa nyingi zinaonesha ajali za mara kwa mara zinazotokea wakati wa uendeshaji na hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi na mali.

Ajali za TRC zimegawanyika katika makundi makubwa matatu:

  1. Uchakavu au ubovu wa vitendea kazi (defective or failure of rolling stock),
  2.  Uchakavu au ubovu wa miundombinu ya reli (defects on track, signaling, mataruma , reli, vifungashio nk), na
  3. Makosa ya kibinadamu (human errors).

Katika mgawanyo huo, asilimia zaidi ya 90 ya ajali hizo, ziko katika kundi la makosa ya kibinadamu ikiwemo kutokuzingatia maelekezo ya miongozo undeshaji wa treni na kutofuata majukumu yaliyoainishwa kwenye vitabu vya miongozo (Engineering Manual and General Rules).

Hivyo, madhumuni ya mafunzo haya mafupi ni kuwakumbusha wafanyakazi juu ya wajibu wa utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku kwa mujibu wa taratibu sahihi kama zinavyoelezwa kwenye miongozo yenu ya kazi (General Rules). Kila mmoja akizingatia utendaji sahihi wa majukumu yake, LATRA tunaamini ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu zitapungua kwa kiasi kikubwa sana. Hivyo itapunguza hasara zinazopatikana kutokana na kupoteza mindombinu na vitendea kazi (rolling stock).

Mafunzo kama haya ni muhimu sana kuwa yanafanyika mara kwa mara na ikiwezekana kuwafikia wafanyakazi wote (Safety Critical Workers) wote. LATRA imekuwa ikifanya kaguzi za mara kwa mara katika kuboresha usafiri wa reli.

Tunaamini kuwa, makosa ya kibinadamu yakipungua TRC itafanya uendeshaji wake kwa usalama na hivyo kufikia malengo yake.

Tunawaomba mkazingatie kufanya kazi kwa bidii na maarifa pia kutumia viwango sahihi kama vilivyoainishwa kwenye miongozo ya TRC na sheria.

Tunapokaribia kuanza uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR), viwango vinavyohitajika vitakuwa ni vya juu sana kwa hiyo ukosefu wa kufuata maelekezo utapelekea kutokea madhara makubwa na kusababisha hasara kwa taifa.

LATRA inaamini kuwa mkizingatia maelekezo ya mtakayopata kwenye mafunzo haya, mtapunguza kwa kiasi kikubwa ajali zitokanazo na makossa ya kibinadamu (human error) na hivyo kutimiza lengo la usafiri bora na salama.

Huduma bora bila ajali inawezekana.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Ninatamka kuwa mafunzo haya yamefunguliwa rasmi.

 

CPA Habibu J. S.  Suluo

Mkurugenzi Mkuu

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA

 

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo