Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI, MHESHIMIWA PROF. MAKAME MNYAA MBARAWA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24
22 May, 2023 Pakua

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyochambua utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya mwaka wa fedha 2022/23, ninaomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea na kujadili Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23. Aidha, ninaliomba Bunge lako tukufu liridhie kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023/24.

2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana leo. Ninamuomba Mwenyezi Mungu atuongoze vyema katika kujadili Hotuba hii ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na bajeti nzima kwa ajili ya kutuwezesha kuwahudumia Watanzania wenzetu.

Pakua Hotuba

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo