Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

LATRA Logo

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu kwa Waandishi wa Habari
Imewekwa: 27 Jul, 2022

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilianzishwa kwa Sheria Na. 3 ya Mwaka 2019 ili kudhibiti huduma za usafiri ardhini katika sekta za reli, barabara na waya. Sheria ya LATRA ilifuta Sheria Na. 9 ya mwaka 2001 iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

LATRA ilianza kutekeleza rasmi majukumu yake tarehe 29 Aprili, 2019 baada ya Sheria yake kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 358 la tarehe 26 Aprili, 2019.

LATRA inaongozwa na Bodi ya wakurugenzi, Menejimenti inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu. Muundo wa Mamlaka una idara tano na vitengo vitano. Aidha, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, Mamlaka ina ofisi katika mikoa yote Tanzania Bara.

Pakua taarifa kamili

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo