15 May, 2023
3:00 asubuhi
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius NyerereDar es Salaam
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) inawaalika wadau wote wa usafiri ardhini waliopo kanda ya Kaskazini kuhudhuria mkutano wa kupokea maoni kuhusu Rasimu za Kanuni Mpya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) utakayofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi, tarehe 19 Mei, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.
Rasimu za kanuni hizi zinapatikana kupitia anwani https://www.latra.go.tz/ . Wadau wote mnaombwa kuhudhuria mikutano hiyo bila kukosa.
Wadau watakaoshindwa kushiriki vikao hivi, wanaweza kutuma maoni yao kwa baruapepe group.maoni@latra.go.tz mpaka tarehe 26 Mei, 2023.